Makonda Amgeuzia Kibao Mwanafunzi anayedai alitekwa
Mar 9, 2018
  • 141,877
  • 380
  • 187


Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda amewataka Polisi wa Mkoa wa Iringa wakimaliza kushughulika na mwanafunzi aliyesema ametekwa wampeleke Dar kwa maana ameuchafua mkoa. Aidha, amewataka Waandishi wa Habari waangalie taarifa wanazopeleka kwa umma, kama hazijathibitishwa na mamlaka husika waachane nazo. Amtaka Kamanda Mambosasa na Jeshi la Polisi kutembea kifua mbele, bila ya kuwepo kwa mtu wa kuwafedhehesha wala kuwanyong'onyesha

Makonda amesema "Watu wanahangaika kwenye mitandao ya kijamii kutukana viongozi na kuhamasisha maandamano, nawapa pole sana. Watafanya hivyo labda mie nikiondoka lakini sio nikiwa mkuu wa mkoa". Amemuagiza Kamanda Mambosasa washughulike kwa mujibu wa sheria na mtu yeyote atakayesimama na kutukana viongozi hasaa kiongozi wa nchi ambaye ni Nembo ya nchi. Ameongeza kuwa "amani ya mkoa wa Dar ni muhimu sana na lazima tujue wengine wakipiga kelele wakaandikwa kwenye front page za magazeti ndio wanapata donors kutoka kwa mataifa yasiyotutakia amani"